Serikali za kaunti zimetakiwa kuweka mipangilio bora ya jiji/miji kama njia moja ya kufanikisha miradi za maendeleo. Akizungumza kwenye warsha moja jijini Kisumu, naibu mkurugenzi wa maswala ya mipango katika wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya miji Timothy Mwangi amesema, kuwepo kwa mpangilio bora wa miji kutawavutia waekezaji kuekeza katika kaunti zote humu nchini. Mwangi amesema serikali kuu na ile za kaunti zinapasa kuweka mikakati, kuhusu namna ya kukabiliana na idadi kubwa ya watu wanaohamia mijini kila uchao; na lengo la kutafuta ajira. Ametahadharisha serikali za kaunti dhidi ya utumizi mbaya wa rasilimali walizonazo, jambo ambalo anahofia huenda ikaongeza kiwango cha umaskini humu nchini.