Mfanyibiashara maarufu katika Kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal, amemkashifu Gavana wa Mombasa Hassan Joho kutokana na ripoti iliyotolewa na Wizara ya Fedha kuhusu jinsi magavana walivyotumia bajeti waliotengewa.
Shahbal, ambaye pia ni mpinzani mkali wa Gavana Joho, alisema kuwa sio jambo nzuri kwa gavana huyo kutumia asilimia 80 ya bajeti hiyo, katika kulipa mishahara na kuendeleza maisha ya kifahari ya maafisa wa kaunti, huku akitumia asilimia 20 pekee kwa maendeleo.
Aidha, mfanyibiashara huyo pia aliikosoa serikali ya Joho kwa kuzipa kipaumbele mambo yasiyofaa kama ziara za kuenda nje ya nchi, badala ya kufanya maendeleo.
“Niliamua kuwania kiti cha ugavana ili kukomboa hali ya uchumi katika Kaunti ya Mombasa, kwa vile Gavana Joho ameshindwa kuendesha kaunti inavyostahili,” alisema Shahbal.