Mgombea wa kiti cha ugavana Kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal ameitaka serikali kuu kuzindua mbinu mpya za kukabiliana na walanguzi wa mihadarati.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza kwenye kikao na wanahabari katika makao makuu ya chama cha Jubilee jijini Mombasa, Shahbal alisema akiteuliwa kuwa gavana, atashinikiza serikali kuunda sheria ya kuwanyonga walanguzi wa dawa za kulevya ili kudhibiti biashara hiyo hasaa katika eneo la Pwani.Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kuangamiza janga hilo.“Iwapo watanyongwa basi walanguzi wote watakoma kuendeleza biashara hiyo haramu,” alisema Shahbal.Aidha, ameongeza kuwa mali zote za washukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya zinafaa kuchukuliwa na serikali ili kutumika katika kupiga vita biashara hiyo.“Mali zao zinafaa zichukuliwe na kutumika katika kuangamiza ulanguzi wa dawa za kulevya,” aliongeza Shahbal.Wakati huo huo, Shahbal amekashifu wanasiasa wa chama cha ODM kwa kuingiza siasa katika vita dhidi ya mihadarati nchini.Amewataka wanasiasa wote kuacha kukashifu zoezi hilo na badala yake kushirikiana katika kuangamiza janga hilo.Aidha, aliikashifu serikali ya kaunti ya Mombasa pamoja na ile ya kitaifa kutokana na juhudi chache wanazofanya kuwaokoa waraibu wa dawa za kulevya.Alisema kuwa kuna takriban watu 60 ambao wanahusishwa na ulanguzi wa mihadarati nchini ambao serikali inatarajiwa kuwaweka wazi ili wachukuliwe hatua za kisheria.  

Photo caption: Mgombea wa kiti cha ugavana Kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal katika hafla ya awali.

Photo source: citizentv.co.ke