Afisa wa upelelezi amejipata kwenye panda shuka baada ya kushindwa kuieleza mahakama ni nani mmiliki wa kamera na kanda ya video inayotumiwa kama ushahidi kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili Mwakilishi wa Wanawake katika Kaunti ya Mombasa Mishi Mboko.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Shahidi huyo, Benjamin Mwaliko, ambaye ni afisa wa upelelezi, alijipata matatani baada ya kutakiwa na mawakili wa utetezi wakiongozwa na wakili Gerad Magolo, kuweka wazi ripoti kuhusu kanda ya video inayo maneno ya uchochezi yanayodaiwa kutamkwa na Mboko.

Haya yanajiri baada ya kanda hiyo ya video kuchezeshwa katika mahakama ya Mombasa kama ushahidi siku ya Alhamisi.

Mboko anadaiwa kutamka maneno hayo yanayodaiwa kuchochea jamii mnamo Juni 1, 2014 wakati wa sikukuu ya Madaraka.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Mei 12, 2016.