Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi katika hafla ya awali. [Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Shahidi katika kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amedai kuwa mbunge huyo aliongezewa kura 262 katika uchaguzi wa Agosti 8.Kulingana na fomu 35B iliyowasilishwa mahakamani, Mwinyi alipata kura 31,584 kinyume na kura 31,322 ambazo zilitumwa kwenye mtandao wa matokeo ya Tume ya IEBC.Akitoa ushahidi huo mbele ya Jaji Njoki Mwangi siku ya Alhamisi, aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge wa Changamwe kwa chama cha Jubilee Abdi Daib aliitaja hatua hiyo kama njama ya wizi.“Huu ni wizi wa wazi uliofanyika katika vituo vingi eneo la Changamwe ili kumpitisha Omari Mwinyi,” alisema Daib.Ushahidi wake ulionyesha kuwa kura zilizoharibika kulingana na Fomu 35B ni kura 494, kinyume na zile zilizo tumwa kwenye mtandao wa IEBC ambao unaonyesha kura 1,120.Daib alitilia shaka tofauti hiyo na kuitaja kama njama ya wasimamizi wa kura hizo kutekeleza wizi.“Tofauti hii ni ishara kuwa uchaguzi huo haukuwa wa uwazi na huru,” alisema Daib.Aidha, picha na nakala ya kifaa cha KIEMS zilizowasilishwa mahakamani zilionesha tarehe ya uchaguzi kuwa Januari 2, 2009 wala sio Agosti 8, 2017.Daid pia alidai kuwa mawakala wake 25 walitimuliwa kitoka vituo 25 vya kupigia kura kama vile kituo cha shule ya msingi ya Bomu, Baraka Village na Shule ya msingi ya Chaani, miongoni mwa vituo vingine.“Mawakala wangu wengi walifurushwa vituoni pasi sababu yoyote mwafaka. Hii ilikuwa ni mjama ya wasimamizi wa uchaguzi kutekeleza wizi wa kura,” alisema Daib.Vile vile aliwasilisha mahakamani picha mbili za vijana waliokuwa wamebeba mfuko wa plastiki pamoja na begi zilizodaiwa kuwa na karatasi za kura zilizokuwa tayari zimetiwa alama, wakiingia katika kituo cha Chaani.Daid alidai kuwa vijana hao waliruhusiwa kutumbukiza karatasi hizo kwenye sanduku la mbunge.“Vijana hawa walirusiwa kutumbukiza karatasi hizo pasi kuzuiliwa na wasimamizi wa kituo hicho cha kupigia kura. Huu ni wizi wa wazi,” alisema Daib.Kesi hiyo itaendelea Machi 2, 2017.