Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Shahidi mmoja katika kesi ya kuchunguza kifo cha raia wa Uingereza aliyepatikana na mihadarati ameiambia Mahakama kuwa Muingereza huyo alifariki akiwa amefungwa pingu mikononi.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Richard Odenyo katika Mahakama ya Mombasa siku ya Jumatatu, afisa wa polisi Issa Saidi alisema kuwa raia huyo wa Uingereza, Alexender Monson, alifariki katika Hospitali ya Diani Palm.Monson alifariki tarehe Mei 19, 2012 katika hospitali hiyo baada ya kubugia dawa za kulevya. Hii ni baada ya kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi wa kituo cha Diani akiwa na mihadharati.Said aliiambia mahakama kuwa hawakuweza kumfungua Monson pingu hizo kutokana na kanuni za polisi hasa kuhusu wahalifu.Tayari mashahidi 21 wametoa ushahidi wao, huku wengine 20 wakitarajiwa kutoa ushahidi wao kuhusiana na kifo cha Monson.Kesi hiyo itaendelea siku ya Jumanne, October 3, 2017.