Balozi wa kudumu wa umoja wa mataifa ‘habitat’ Sam Ongeri amesema shamba alilopata katika mji wa Kisii ni la halali.
Alikuwa akiongea wakati alipokuwa anahojiwa na kuchunguzwa na bodi ya ardhi nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Muhammed Swazuri kueleza jinsi alipata shamba hilo lake Ongeri alisema hakunyakuwa shamba bali alifuata utaratibu unaofaa ili kupata shamba hilo.
“Mimi niliwai kuwa waziri katika wizara mbalimbali singetumia fursa hiyo kunyakua mashamba ya serikali kila shamba ambalo niko nalo haswa hapa Kisii nililipata kwa njia ya halali,” alikiri Ongeri.
Wengi wa mabwanyenye wanaendelea kuchunguzwa ili kubaini jinsi walipata mashamba mjini kisii.
Hii ni baada ya serikali kugundua kuwa mashamba yao yamenyakuliwa hivyo basi kuanzisha vikao vya uchunguzi mjini Kisii katika vikao ambavyo vitakamilika siku ya Ijumaa wiki hii.