Sherehe ya kufana ya harusi kati ya Nelson Mandela na Lydia Akinyi Jumatatu huko Lord Egerton Castle, Ngata ilisitishwa kwa muda baada ya maharusi kufungiwa kimakosa katika chumba kimoja. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Hali ya taharuki ilitanda baada ya mwongoza ratiba kutangaza kwamba; "maharusi wameshindwa kutoka baada ya bawabu kufunga mlango kimakosa na kupotea na ufunguo."

Ililazimu wachungaji wa dhehebu la SDA waliofika kusimamia harusi hiyo kuingilia kati ili kutatua swala hilo. 

Baada ya lisaa limoja, maharusi walifunguliwa mlango na kumaliza wasiwasi iliyokuwepo.

Hata hivyo, maharusi hayo waliomba msamaha kwa hitilafu hiyo.

"Ningependa kuomba msamaha kwa kuchelewesha ukataji wa keki kwani haikuwa makosa yetu bali ni bawabu aliyekosea,"alisema Mandela. 

Harusi hata hivyo iliendelea vyema na kukamilika majira ya saa kumi na moja jioni. 

Japo hapakukosa semi mbali mbali kutoka kwa waliohudhuria.