Waziri wa Elimu nchini Dkt Fred Matiang’i imeshinikiza kutumika kwa sheria mpya alizozidhinisha ili kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inakabiliana kikamilifu na changamoto zinazoshuhudiwa katika sekta hiyo.
Dkt Matiang’i amesema kuwa ni lazima kwa wadau wote wa sekta ya elimu kushirikiana katika kufanikisha sheria hizo ili maswala ya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa kudhibitiwa.
Akiongea na wanahabari mjini Mombasa baada ya kufungua rasmi kongamano la muungano wa walimu wakuu nchini, Matiang’i amesema kuwa wizara ya elimu itazidi kupiga marufuku mikutano ya maombi na ziara za wazazi na jamaa za wanafunzi kama njia moja wapo ya kuzuia wizi wa mitihani katika muhula wa tatu.
Wakati uo huo amedai kuishinikiza serikali kutenga shilingi bilioni 7 kwa sekta ya elimu zitakazogharamikia uboreshaji wa majengo ya shule na vifaa vya kisasa vya masomo ili kuimarisha sekta ya elimu na matokea bora zaidi ya mitihani.
Kongamano hilo la muungano wa walimu wakuu la siku mbili linatarajiwa kujadili zaidi maswala ya umarishaji wa sekta ya elimu, kudhibiti wizi wa mitihani na migomo ya wanafunzi ya kila mara shuleni.