Kijana mmoja amehukumiwa miezi miwili jela kwa kosa la kumshambulia mamake kwa kumpiga mawe.
Mshtakiwa huyo, Rama Sadi, anadaiwa kutekeleza kisa hichi siku ya Jumatatu katika eneo la Changamwe.
Aidha, anadaiwa kuwafungia chumbani wadogo zake pasi sababu zozote.
Sadi alikubali kosa hilo mbele ya Hakimu Daglous Ogoti siku ya Jumanne.
“Nakubali kosa langu, ila naomba msamaha kwani shetani ndie alinishawishi kutekeleza kisa hicho,” alisema Rama.
Hakimu Ogoti alimpa Rama siku 14 kukata rufaa.