Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika linataka kuchukuliwa hatua za kisheria polisi waliowapiga na kuwajeruhi waandamanaji wa Cord.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khallid amesema ni kazi ya polisi kulinda usalama wa raia wala si kuwashambulia pasi makosa.

Aidha, siku ya Jumanne, aliongeza kuwa sheria haijawapatia ruhusa ya kutumia nguvu kupita kiasi, na kutaja tukio la siku ya Jumatatu kama ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Hii ni baada ya kijana aliyeonekana akipokea kipigo kutoka kwa maafisa wa polisi kuripotiwa kuaga dunia.

Kauli hii inajiri baada ya wafuasi wa Cord katika kaunti ya Nairobi na Kisumu kujeruhiwa kwenye maandamano ya kutaka kubanduliwa kwa makamishena katika tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini kabla ya uchaguzi mkuu ujao yanayoongozwa na mrengo wa Cord.