Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Agenda HURIA linashirikiana na serikali ya kaunti ya Mombasa katika mpango wa kuwasaidia vijana na familia za mitaani.
Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Ijumaa, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Yusuf Lule Mwatsefu, alisema kwa muda mrefu, familia hizo za kurandaranda mitaani zimetengwa na jamii, na kwamba kuna haja zisaidiwe.
Lule, alieleza kuwa idadi kubwa ya watoto wa kurandaranda mitaani inachangia kukithiri kwa changamoto za kiusalama na visa vya uhalifu.
“Tumeona tushirikiane na serikali ya kaunti ya Mombasa kuhakikisha kuwa tunawasaidia watoto wa kurandaranda mtaani ili tuwakinge na maswala ya kihalifu,” alisema Lule.
Kwa upande wake mkurugenzi wa maswala ya vijana, jinsia na michezo katika kaunti ya Mombasa Esther Ingolo, alisema kuwa Serikali ya kaunti hiyo italiunga mkono kikamilifu shirika hilo kwa kulitafutia wadau zaidi wa kuufandili mpango huo.
“Kama serikali sisi tumeamua kufanya kazi na Shirika la Huria kuunga mkono kikamilifu juhudi zao pamoja na kuwatatutia wafadhili kufanikisha lengo lao, alisema Esther.