Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limeelezea wasiwasi wake kuwa huenda kukazuka vurugu katika uchaguzi mkuu ujao iwapo wanasiasa wanaoeneza jumbe za chuki hawatathibitiwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea mjini Mombasa siku ya Jumatatu, afisa wa maswala ya haki na sheria katika shirika hilo Francis Auma Gamba amesema kuwa ongezeko la matamshi ya chuki baina ya wanasiasa linatia wasiwasi.

Ameitaka Tume ya kitaifa ya uiano na utangamano nchini NCIC kukabiliana na swala hilo ili kupunguza hofu ya kuzuka kwa vurugu nchi wakati Wakenya wanapoelelea kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Auma aidha ameitaja tume hiyo inayoogozwa na mwenyekiti wake Francis Ole Kaparo kama isiyowajibika kwa kutowachukulia hatua wanasiasa au watu wanaotoa matamshi ya chuki hadharani na hivyo basi akaitaka iwachukulie hatua wanasiasa wanaotoa jumbe za chuki hadharani ili wakabiliwe na sheria.

"Tunaitaka tume ya NCIC kuhakikisha kuwa inawachukulia hatua kali za kisheria wananchi na wanasiasa wanaotoa matamshi ya chuki ili kuhakikisha kuwa taifa hili linakuwa huru hata wakati  wa uchaguzi mkuu ujao," alisema Auma.