Shirika la Metro Child World limetaka wanaoendeleza dhuluma dhidi ya watoto katika kaunti ya Nakuru na taifa kwa jumla kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanaharakati Jeanne kutoka shirika hilo anasema kuwa katika karne hii, ni jambo la kusikitisha kwa watoto kudhulumiwa.

"Karne hii mtoto hafai kudhulumiwa bali tunafaa kuhakikisha wanalindwa na wanapata haki ya elimu" Jeanne alisema.

Alikuwa akizungumza katika shule ya msingi ya Crater mjini Nakuru wakati wa hafla ya kushukuru kwa matokeo mema.

Wakati huo huo ameongeza kuwa kama shirika watazidi kupiga jeki watoto katika maswala ya elimu.