Shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Mombasa limeenda makongamano ya kuwahamasisha vijana ambao hawajajitosa katika jinamizi la mihadatari ili kuzuia kuangamia kwa vijana wengi.
Afisa mkuu wa shirika hilo kaunti ya Mombasa Mohamed Rajab amesema kuwa watahakikisha wanashirikiana na viongozi wa kaunti ya Mombasa ikiwemo mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir kuwahamasisha jamii.
Akizungumza katika eneo la Mvita mjini Mombasa siku ya Jumanne, Rajab amesema kuwa wamechukua hatua hiyo kufuatia kuongezeka kwa idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya na juhudi hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti utumizi wa mihadarati.
"Tumepanga kushirikiana na viongozi na wadau wengine kuhakikisha kuwa maswala ya utumizi wa mihadarati tunakabiliana nayo ili kuwasaidia vijana wetu kujitosa katika jinamizi hilo," alisema Rajab.
Wakati uo huo amewapa changamoto vijana kukoma kukaa maskani na badala yake kujihusisha katika maswala ya kimaendeleo.