Shirika la Msalaba Mwekundi kaunti ya Mombasa limebaini kudhibiti kwa kiasi kikubwa ongezeko la ugonjwa wa Homanyongo Mombasa kwa kushirikiana na serikali ya kaunti ya Mombasa.
Afisa mkuu wa shirika hilo Mohammed Rajab Said, amesema kuwa kutokana na juhudi kubwa ambazo shirika hilo limefanya hasa kuwashauri wakaazi kutumia maji safi sambamba na kutibu maji ya visa ripoti ya kuonyesha kuenea kwa maradhi yao imedhibitiwa.
Amesema kuwa kama shirika litahakikisha kuwa linatibu maji yote katika kaunti hiyo huku likiwashikiza wakaazi kuzingatia usafi wa mazingira huku pamoja na kuhakikisha kuwa maeneo wanayoishi yako safi ili kuzuia kuchipuka wa maradhi hayo tena.
Afisa huyo hata hivyo amesema kuwa licha ya zaidi ya visa 80 kuripotiwa katika kaunti ya Mombasa ya wakaazi kuambukizwa maradhi hayo kwa kiasi kikubwa, wamefanikiwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo wa Homanyongo.
"Tunaweza kusema kuwa tumefaulu kutibu maji yote kaunti ya Mombasa na kutokana na hilo basi ripoti ya kuongezeka kwa visa vya maradhi ya homanyogo imepungua kwa asilimia kubwa hivyo basi tunazidi tu kusisitiza wakaazi wazidi kutumia maji safi ili kuzuia kuenea kwa maradhi mengi ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya maji machafu," alisema Rajab siku ya Jumanne mjini Mombasa baada ya kutembea maeneo ya wakaazi.