Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika la msalaba mwekundu tawi la Nakuru linasema takriban familia 17 katika eneo la Kwa Rhonda viungani mwa mji wa kaunti hiyo zimeaachwa bila makao kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikishuhudiwa kwenye eneo hilo.

Mratibu wa shirika hilo tawi la Nakuru James Gichimu aliratibu hayo kwenye mahojiano na mwandishi huyu Jumatano akikariri kwamba wako katika harakati za kuzisaidia familia hizo.

‘Tumetadhmini hali ilivyo katika mtaa wa Kwa Rhonda tukapata familia 17 zimeadhirika na nyumba zao zimesombwa na maji. Imebidi watafute mahala pengine pakuishi. Tuliwapelekea msaada kama vile blanketi, sabuni na sufuria miogoni mwa vitu vingine,’ alisema Gichimu.

Pamoja na hayo, alisema familia zingine 74 pia zimeathirika na mvua hizo kwenye eneo la Mwariki huku akiongezea kuwa tayari, shirika hilo limetoa msaada kwa familia hizo.

‘ Tulienda upande wa Mwariki na tukapata maji yalkuwa yameingia katika nyumba 74. Hata hivyo, waliweza kuondoa maji hayo na kurudi kwenye nyumba hizo,’ alisema Gichimu.

Wakati huo huo, mratibu huyo ameweka bayana kwamba wanashirikiana na serikali ya kaunti ya  kuhakikisha kuwa waathiriwa wote wa mvua hizo wanapata misaada ya kibinadamu.

Ni matamshi yanayojiri huku wakaaz wa maeneo mengine kwenye kaunti hiyo wakiathirika kutokana na mvua ya gharika ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika maeneo hayo katika siku za hivi karibuni.