Watotonyatima na watoto kutoka jamii zisizojiweza katika jamii mjini Nakuru wana kila sababu ya kuendeleza elimu na kupata mafunzo katika maswala ya hoteli baada ya shirika la Ujima Foundation kuanzisha mpango maalumu. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika hilo limekuwa likitoa mafunzo ya taaluma kwa watoto yatima lakini sasa wameanza kupeana mafunzo ya hoteli kwa watoto yatima na watoto kutoka familia maskini. 

Katika mahojiano ya kipekee na mwanahabari huyu siku ya Ijumaa, afisa wa uhusiano mwema katika shirika hilo Charity Runnoh alisema kuwa waliamua kuanzisha mpango huo ili kuimarisha jamii. 

"Tumekuwa tukifanya na mayitima lakini sasa tumeanza kujumuisha hata wale watoto wenye wanatoka familia maskini ili kuhakikisha wanaendelea maishani," alisema Charity. 

Aliongeza kuwa shirika hilo lenye makao yake Nakuru linajizatiti kuhakikisha kwamba swala la umaskini linatokomezwa katika jamii. 

Hata hivyo, aliongeza kuwa changamoto kuu ni kuwatafutia ajira baada ya kupata mafunzo ya maswala ya hoteli. 

"Inakuwa changamoto hawa wanafunzi wakifuzu kupata ajira lakini tunajaribu kuzungumza na hoteli za hapa Nakuru ili kupata nafasi," alisema. 

Wakati uo huo, Charity Runnoh alitupa wito kwa serikali na wahisani wengine kupiga jeki mashirika na washikadau katika sekta ya elimu. 

Kwa mujibu wake, ni hatua hiyo tu itakayookoa jamii.