Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Madai ya hivi majuzi ya Naibu Gavana wa Kaunti ya Nyamira Amos Nyaribo, kuwa shirika moja lisilo la kiserikali linatumika na Seneta Kennedy Okong'o, kuhujumu uongozi wa Gavana John Nyagarama yameshtumiwa na shirika hilo.

Akiongea katika eneo la Nyandoche Ibere siku ya Jumatatu wakati wa hafla yakukutana na wakulima, mshirikishi wa shirika la African Development Group Bw Emmanuel Moguche, alisema kuwa kamwe shirika hilo halijajihusishi na maswala ya kisiasa ila nia yao nikupunguza viwango vya umaskini miongoni mwa jamii za Africa.

"Ni jambo lakushangaza kwamba viongozi wa hadhi ya naibu gavana wanaweza tuhusisha na siasa zakuhujumu uongozi wa Gavana Nyagarama, huku majukumu yetu yakifahamika waziwazi. Yafaa serikali ya kaunti iheshimu kuwepo kwetu hapa Nyamira kwa kuwa hili ni shirika lenye mizizi kote Africa na lenye nia yakuangamiza umaskini," alisema Moguche.

Afisa huyo alisema kuwa shirika hilo lipo tayari kufanya kazi na serikali ya kaunti hiyo.

“Ikifikia swala lakufanya maendeleo, yafaa tuweke tofauti zetu kando na kufanya kazi pamoja kwa minajili ya kuangamiza umaskini nakuimarisha maendeleo miongoni mwa jamii,” alisema Moguche.