Shughuli za usafiri katika kivuko cha feri cha Likoni ilitatizika kwa muda mfupi Alhamisi asubuhi baada ya feri moja kukosa mwelekeo na kusimama mahali pasipo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na usimamizi wa shirika la huduma za feri KFS, feri hiyo ya Mv Kwale ilipata matatizo ya kimitambo wakati ilipokuwa ikielekea upande wa kisiwani mwendo wa saa mbili asubuhi.

Shirika hilo lililazimika kuleta usaidizi wa Mv Nyayo na boti la huduma za dharura kupunguza watu katika feri hiyo na kuwavusha hadi kisiwani.

Kwa sasa feri tatu zina hudumu katika kivuko hicho.

Abiria waliokuwa kwenye feri hiyo walilazimika kusuburi usaidizi kwa zaidi ya lisali moja.

“Tumekaa kwa zaidi ya saa moja baharini baada ya feri yetu kukwama hadi tukapata usaidizi kutoka kwa Mv Kwale. Hata hivyo, tunashukuru tumetoka salama,” alisema Said Athman, mmoja wa wasafiri.