Mmoja wa mashujaa kutoka Kitutu Chache Kusini, Kaunti ya Kisii ameipongeza serikali kwa kuwatambua kwa juhudi zao za kupigania nchi ya Kenya ili kupata Uhuru kutoka kwa wakoloni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Peter Bogongo, mmoja wa wakilishi wa mashujaa kutoka eneo bunge la Kitutu Chache, alimpongeza Gavana James Ongwae kwa kuwahakikishia kuwa maslahi yao yataanza kuangaliwa.

Shujaa huyo alikuwa akiongea Jumatatu baada ya maadhimisha siku kuu ya Madaraka ambayo iliandaliwa kwenye uga wa michozo wa Gusii Green ambapo gavana Ongwae aliongoza wakaazi, viongozi mbalimbali kutoka serikali kuu na ile ya kaunti kusherehekea siku hiyo.

Wakati huo huo Ongwae aliweza kuwaahidi wale mashujaa wote si tu waliopigania uhuru bali wote walioitambulisha nchi ya Kenya katika nyanja za kimataifa ambapo gavana huyo alimtambulisha mwanariadha mkongwe kwa hadhara ilioshiriki hafla hizo.

Iwapo mswada ulioko kwenye bunge kaunti ya hiyo utapitishwa mashujaa wote kwenye Kaunti ya Kisii wakiwemo wanasoka, wanariadha na waliopigania uhuru wa nchi watakuwa wanalipwa pesa kidogo za kuwaendeleza kimaisha na wengine kutambuliwa kwenye barabara za kaunti.