Mamlaka ya Umeme nchini REA, imeahidi kuweka umeme katika shule za umma ili kuhakikisha kuwa elimu inaimarishwa mashinani.
Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Dkt Simon Gicharu, amesema kuwa tayari shule za umma elfu 23 zimenufaika kutokana na mradi huo.
Gisharu alisema kuwa hatua hiyo itawawezesha wanafunzi kusoma hadi masaa ya jioni, kama njia moja wapo ya kuinua viwango vya elimu nchini.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumanne, Gicharu alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kudhibiti changamoto zinazoshuhudiwa kwa sasa katika shule za umma, hasaa zilizoko mashinani.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama kwa serikali.
"Mradi huu tuliopewa na serikali utahakikisha kuwa shule zote za umma nchini hata kule mashinani zinapata umeme ili kuimarisha viwango vya elimu,” alisema Gicharu.
Aidha, alisema kuwa mradi wa kusambaza vipatakilishi kwa shule za umma nchini unaotekelezwa na serikali kuu utafanikishwa kwa urahisi kupitia mradi huo.