Shule zote ambazo zinafanya vyema katika mitihani ya kitaifa zitapata ufadhili mkubwa kutoka kwa serikali ya kitaifa.
Akizungumza mnamo siku ya Jumatano katika shule ya upili ya wavulana ya Kisii High kwenye mkutano wa walimu wakuu wa shule zote katika eneo hilo, Waziri Fred Matiang’i alisema haiwezekani shule hazifanyi vyema kisha zinaomba ufadhili haswa maktaba za vitabu na mahitaji mengine huku akisema kila shule inastahili kutumia kile ilicho nacho kwanza.
“Mimi kama waziri siwezi kufadhili shule ambayo iko karibu na kwangu kwa sababu iko karibu na nyumbani kama hjaifanyi vyema siwezi kabisa,” alisema Matiang’i
"Shule zile zinafanya vyema katika mitihani ya kitaifa zitapata ufadhili mkubwa kile ninasema shule yako inapofanya vyema ufadhili unainuika zaidi,” aliongeza Matiangi.
Wakati huo huo, Matiangi alisema serikali ya kitaifa kwa miaka mitatu iliyopita imetoa vitabu vya kusoma vinavyogharibu zaidi ya shilingi billion 1.36 kwa shule za upili 346 zilizoko katika kaunti ya Kisii na kusema hakuna haja kwa shule kutofanya vizuri katika mitihani.