Wanafunzi katika shule kadhaa eneo bunge la Molo wamefaidika na ufadhili wa kimasomo kutoka kwa rais.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kupitia kwa mradi wa basari ya rais, wanafunzi kadhaa walifadhiliwa kupata masomo.

Wale waliopata msaada huo ni walio na changamoto za kimaubile pamoja na mayatima.

Mbunge wa Molo Jacob Macharia alikabidhi shule za eno bunge hilo cheki hizo hii leo ili kuhakikisha wanafunzi hao wamefadhiliwa ipasavyo.

Macharia aliwataka wanafunzi waliofaidika kuhakikisha kuwa wamejitahidi na kutia bidii. Shule ambazo zilifaidika ni Molo Secondary, Njenga Karume, Kambala, Mona baadhi ya zingine.