Shule za kibnafsi bado zaendelea na masomo ya likizo ya mwezi huu, baada ya wanafunzi kadhaa kuonekana wakienda shuleni kwa masomo hayo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Nilipozungumza na meneja wa shule moja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa wao wataendelea na masomo yao kwa mda.

"Sisi kama wenyeji wa shule za kibnafsi tuna jukumu la kujilipa mishahara sisi wenyewe, hatuoni haja ya serikali kutukazia sana ilihali serikali haitulipi," alisema meneja huyo. 

Kaunti ya Nyamira ina idadi kubwa ya shule zinazoendesha masomo hayo ya likizo, na akithibitisha hayo, afisa wa elimu katika kaunti hiyo aliwaonya wanaokiuka sheria zinazosimamia masomo hayo kuwa huenda wakachukuliwa hatua za kisheria kama hawatasitisha masomo hayo.

"Tutawachukulia hatua za kisheria hao ambao wanaendesha masomo ya likizo kwa kutotii sheria za katiba ya Kenya," alisema afisa huyo. 

Wanafunzi wengi huenda wakaachaa kuhudhuria masomo hayo baada ya wazazi wao kuonywa kuwa mwanafunzi yeyote atakayepatikana akienda kuhudhuria masomo atatiwa mbaroni.