Shule ya msingi ya Echoro iliyoko wadi ya Gesima kaunti ya Nyamira itafadhiliwa vitabu vya kudurusu juma lijalo ili wanafunzi wa darasa la nane kuvitumia kujitayarisha katika mtihani wa kitaifa, KCPE mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Ijumaa, aliyekuwa mwalimu na aliyestaafu katika wadi hiyo Robert Osebe aliahidi kufadhili shule hiyo vitabu hivyo ili wanafunzi hao wa shule hiyo kudurusu mitihani ili kupita katika mitihani ya mwaka huu.
“Wanafunzi hawawezi kupita katika mitihani ikiwa hawana vitabu vya kudurusu ili kujua jinsi maswali yamekuwa yakija katika miaka ya awali,” alisema Osebe.
“Juma lijalo nitafadhili shule ya msingi ya Echoro vitabu hivyo ili viwango vya elimu kuinuka katika wadi ya Gesima,” aliongeza Osebe.
Wakati huo huo, Osebe aliomba washkadau wote wa elimu katika shule hiyo kujiunga pamoja kuhakikisha vitabu hivyo vimelindwa vizuri ili wanafunzi wanaofuata kuvitumia vitabu hivyo kila mwaka wakati wa kudurusu mitihani na kupita