Shule ya Msingi ya Riomanga iliyoko wilayani Masaba kaskazini eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira ilifadhiliwa na talakilishi 10 kutoka kwa afisa mkuu wa benki ya dunia Charles Mochama.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika uga wa shule hiyo ya Riomanga, Mochama alisema ameanzisha mradi wa kufadhili shule za msingi ambazo ziko kwa zone ya Bochari talakilishi kama njia mojawapo ya kuinua viwango vya elimu katika eneo hilo.
Aidha, afisa huyo alisema tarakilishi hizo zitasaidia walimu kutengeneza makaratasi ya maswali ya mitihani ili wanafunzi wawe wakifanyishwa mitihani baada ya kila mwenzi.
“Nawaomba walimu mtie motisha mnapowafundisha wanafunzi. Tarakilishi hizi zitawasaidia kutayarisha maswali ya mitihani, alisema Mochama.
Afisa huyo alishangazwa na kuwa wazazi hawakuhudhuria hafla hiyo ya kufadhili shule hiyo talakilishi ilhali walikua wamealikwa.
“Wazazi kutohudhuria hafla hii ni ishara kuwa watoto wao hawatapita mitihani. Nawaomba wazazi wa eneo hili mnapoalikwa kwa mkutano wowote mhakikishe mnahudhuria mkutano huo,” alisema Mochama.
Aliongezea: “Naomba wale wazazi ambao walikuja hapa leo muwafahamishe wazazi wengine wawe wakihudhuria mikutano wanapoalikwa,”aliongeza Mochama.
Hafla hiyo ilihudhuliwa na mwenyekiti wa chama cha 'Kenya National Union of Teachers' (KNUT) katika wilaya ya Masaba kaskazini Meshack Obonyo ambaye pia aliunga mkono matamshi ya Charles Mochama.