Wanafunzi wa shule za msingi kutoka Wadi ya Mekenene, eneo bunge la Borabu, wana kila sababu yakutabasamu baada ya mwakilishi wa wadi hiyo Bw Alfayo Ngeresa kununu tanki za maji zenye kima cha Sh1.2m ambazo zitsaidia shule hizo kuhifadhi maji.
Akizungumza siku ya Alhamisi kwenye hafla yakupeana mitungi hiyo ya maji katika shule ya msingi ya Highway kule Chepilat, Ngeresa alisema kuwa mradi huo utanufaisha shule tano zaidi, zikiwemo shule za upili.
"Mradi ambao nimeuanzisha hapa hii leo utaonelea kuwa shule zingine tano zitafaidika kupata tanki hizi za maji ili ziwasaidie kuhifadhi maji,” alisema Ngeresa.
Ngeresa alisema kuwa mradi huo utafanikisha uhifadhi wa maji hasa katika msimu huu wa mvua ya El Nino huku akiwasihi wakazi kuchukua fursa hiyo kuhifadhi maji zaidi ili kujiandaa kwa msimu wa ukame mapema mwaka ujao.
Shule zitakazo faidi na mradi huo ni pamoja na Magura, Riosanda, Mwongori, Mekenene na ile ya Highway.