Rais Uhuru Kenyatta amesema siasa za kupotosha ambazo ni za muungano wa upinzani Cord zilisababisha taifa la Uganda kutoshirikiana na Kenya kukarabati mabomba ya kupitisha mafuta.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya taifa hilo la Uganda kuamua kupitisha mabomba ya mafuta katika taifa la Tazania badala ya Kenya jinsi ilivyokuwa inatarajiwa kufuatia sasia za upinzani nchini.

Akizungumza siku ya Jumatano mjini Nyamira wakati wa ziara zake katika eneo la Gusii, Uhuru alisema upinzani umekuwa ukipotosha wananchi kuwa huenda kura za uchaguzi wa mwaka ujao zikakumbwa na changamoto na kusababisha taifa la Uganda kuogopa kushirikiana na Kenya kukarabati mabomba ya mafuta kwa kudai huenda wakapata hasara iwapo rabsha zitashuhudiwa.

“Siasa za upinzani zilifanya Uganda kutoshirikiana nasi kukarabati mabomba ya kupitisha mafuta kwa kudai watapata hasara,” alisema Uhuru.

Kenyatta aliomba upinzani kupiga siasa za sera zinazojenga taifa kbadala ya kupotosha wananchi na kulemaza maendeleo ya nchi kwa jumla.