Mbunge wa Likoni Mwalimu Masoud Mwahima amepinga uvumi unaoeneza na baada ya wanasiasa kuwa sio mwanachama tena wa ODM.
Akizungumza na wanahabari katika eneo bunge lake la Likoni siku ya Jumatano, Mwahima alisema kuwa bado yuko katika chama cha ODM hadi bunge la kitaifa litakapo vunjwa rasmi kwa uchaguzi mkuu ujao.
Mwahima amewakashfu wanasiasa wanaozidi kumshinikiza kujiuzulu na kufanyika kwa uchaguzi mdogo, huku akisema kuwa jambo hilo kamwe halitafanyika hadi bunge la kitaifa litakapovunjwa rasmi kwa uchaguzi.
“Nataka kuwaambia wanasiasa kukoma kueneza uvumi kuwa mimi nimekihama chama cha ODM, bado niko ODM hadi bunge la kitaifa litakapovunjwa rasmi kwa uchunguzi, na ningependa kuwaonya wale wanasiasa kuwa wasichukulia jambo hilo kwa misingi ya kuvuruga watu wa Likoni tunataka kudumisha amani,” alieleza Mwahima.
Hata hivyo, ameahidi kufanya kazi na serikali kuu kuhakikisha kuwa maswala ya kimaendeleo katika eneo bunge la Likoni yanatekelezwa.