Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Nairobi Evans Kidero amesema kuwa shutuma zinazomtaja kuwa alitoa hongo ya shilingi milioni mia mbili zimetokana na hali ya 'kuchanganyikiwa' katika idara ya mahakama.

Huku, tume maalum iliyoteuliwa kuchunguza madai ya kuwa jaji wa mahakama ya juu zaidi Philip Tunoi alipokea hongo hiyo ikitoa ripoti yake Ijumaa alasiri, Kidero alisema kuwa ana  wingi wa matumaini kuwa ataondolewa mashataka hayo.

Aidha amesema kuwa hakuhusika kwa vyovyote kutoa hongo kwani alichaguliwa kwa haki na sasa anaendeleza kazi ya kuijenga Nairobi na ambayo amekuwa akifanya vyema.

"Kama mnavyoniona niko jasiri na najua madai hayo yote ni propaganda na ikiwa nitaitajika kuyasema ninayoyajua bila shaka nitasema," Alisema Kidero.

Gavana huyo alikuwa akizungumza na wanahabari Ijumaa wakati wa mkutano wa wakuu wa kaunti hiyo katika hoteli ya Sawela mjini Naivasha.

Naye spika wa kaunti hiyo Alex Ole Magelo alisema kuwa Kidero hajafanya kosa lolote na kwamba ataondolewa lawama hizo ili aendeleze ujezi wa Nairobi.

"Tunamwomba mungu akuongoze na akuondolee tuhuma hizo na mimi na wawakilishi wote wa kaunti ya Nairobi tutasimama nawe hadi mwisho," Magelo alisema.