Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua amekanusha vikali madai yaliyoibuliwa kwamba anahusika na kundi haramu la Mungiki.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbugua alisema kuwa wanaoeneza uvumi huo ni baadhi ya wanasiasa walio na azma ya kuwania kiti cha ugavana.

Aliwataka wapinzani kutumia siasa komavu pasi kuchafuliana jina.

Kinuthia alikuwa akizungumza Ijumaa katika kikao na wanahabari mjini Nakuru.