Mwakilishi wadi ya Biashara mjini Nakuru Stephen Kuria amekanusha madai kwamba ana uhusiano na kundi la Mungiki.
Hii ni baada ya kundi moja la wafanyibiashara katikati mwa mji kudai kwamba kuna kundi la mungiki lililoshirikiana na MCA Huyo kugawa nafasi za vibanda vya Biashara. Hata hivyo, katika mahojiano ya kipekee Jumatatu, MCA Kuria maarufu kama 'Mhesh' alikanusha madai hayo na kusema kuwa hajawai kuwa na uhusiano na Mungiki.
Kuria alisema kuwa ni yeye binafsi aliyewagawia wafanyibiashara nafasi hizo za vibanda.
"Nashangaa sana wakati wachache wanajitokeza na kueneza propaganda ilihali ni mimi mwenyewe nilitembea katika soko nikiwagawia vibanda na mimi si mungiki"alisema Kuria.
Aliwataka wapinzani wake kutoingiza siasa za propaganda katika maswala ya maendeleo.