Seneta wa Nairobi Mike Sonko anatarajiwa kufika katika Mahakama ya Mombasa siku ya Jumanne kuelezea aliko mwenyekiti wa vuguvugu la MRC.
Hii ni baada ya mwenyekiti huyo, Omar Mwamnuadzi, kususia vikao vitatu vya kesi zinazomkabali.
Sonko amekuwa mdhamini wa Mwamnuadzi tangu kukabiliwa na mashtaka hayo.
Mwamnuadzi na wenzake zaidi ya 20 wanakabiliwa na mashtaka ya kuandaa mkutano kinyume cha sheria na kuwa wanachama wa kundi la MRC.
Majuma mawili yaliyopita, Idara ya polisi Kaunti ya Kwale iliagizwa kumtia mbaroni Mwamnuadzi kwa kususia vikao vya kesi inayomkabili.