Waziri wa ardhi na mipango ya mji katika kaunti ya Mombasa Anthony Njaramba amesema kuwa serikali ya kaunti hiyo ina mikakati ya kubadili taswira ya soko la Kongowea ambayo ni soko kubwa katika kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Njaramba alisema kuwa kuna haja ya maduka ya kisasa kujengwa katika soko hilo ili kuzidisha mapato ya wafanyikazi katika soko hilo huku akisema kuwa biashara katika soko hilo linachangia pakubwa katika uchumi wa serikali ya kaunti hiyo.

“Ni vyema iwapo serikali ya kaunti tutaangazia maaswala ya wanabiashara katika soko hili, angalau wafanyibiashara wapate mahali pazuri pa kufanyia biashara mahali ambapo pana kivuli,” alisema Njaramba.

Aidha, bunge la kaunti ya Mombasa imesema kuwa itatenga fedha katika bajeti ya mwaka huu ili kutekeleza miradi mbali mbali katika soko hilo.