Seneta wa Nairobi Mike Sonko akiwa na aliyekuwa msemaji wa MRC Mohamed Rashid katika kikao cha mahakama hapo awali. Picha/ nation.co.ke
Mahakama ya Mombasa imetakiwa kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kuhusu uhalali wa kundi la MRC.
Akizungumza nje ya jengo la Mahakama ya Mombasa, Seneta wa Nairobi Mike Sonko ameitaka mahakama hiyo kutowanyanyasa wanachama wa kundi la MRC na badala yake kuwaondolea mashtaka yanayowakabili.“Hii ni mahakama ya chini na inafaa kuheshimu uamuzi wa mahakama ya rufaa na kufutilia mbali kesi inayowakabili wanachama wa MRC,” alisema Sonko.Aidha, Sonko lisema kuwa atasalia kuwa mdhamini mkuu wa wananchama hao hadi pale kesi yao itakapokamilika.“Sitaondoa udhamini wangu kwa wanachama wa MRC hadi mwisho wa kesi hii,” alisema Sonko.Sonko amesitiza kuwa yuko tayari kuadhibiwa na mahakama iwapo kiongozi wa kundi hilo Omar Mwamnuadzi hatapatikana.“Niko tayari kuadhibiwa na mahakama na niko tayari kupoteza shamba langu kwa serikali iwapo Mwamnuadzi hatapatikana,” alisema sonko.Kauli hii inajiri baada ya Sonko kutakiwa kueleza aliko Mwamnuadzi baada ya kukwepa vikao vya mahakama.Miezi mitatu iliyopita, Sonko aliomba muda ili kuweza kumtafuta Mwamnuadzi lakini hadi sasa hajulikani aliko.Zaidi ya wanachama 30 wa MRC wanakabiliwa na kesi ya kuendesha mikutano kinyume cha sheria pamoja na kuwa wanachama wa kundi hilo haramu.Kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo kuwa likizoni.