Boss wa Nai Mike Sonko anawaomba wasee wa mtaa wampe advice kabla hajajuchuja works.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kupitia FB, Sonko alidai hataki kuwacha kazi kama 'bro' wake 'yule alihepa job bila hata kuconsult raia waliomuweka ofisini'.

Sonko aliomba advice kabla hajadecide kujikata.

“Lakini pia mujue hii kazi imekua ngumu iko karibu kunishinda na sio mambo ya flag hizo nimekubali kutoa as adviced by Karanja Kibicho na Ndegwa but nitawambia very soon ni kwanini ndio muniadvice iskue kama yule my bro aliehepa bila kuconsult.Kuweni na siku njema yenye mafanikio na baraka tele na Mungu awalinde nyote,” Sonko alisema.

Juzi, kuna raia kwenye twitter walidai kuwa boss wa Nai amekuwa akilala kwa kufanya kazi yake.

Kupitia #FailedGovernorSonko raia walidai kuwa Sonko anafaa kumake sure mitaa zina maji, security pia iko rada na mahawker watoke town.