Seneta wa Nairobi Mike Sonko katika hafla ya awali. Picha/ politics.co.ke

Share news tips with us here at Hivisasa

Seneta wa Nairobi Mike Sonko amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutoa amri ya kukamtwa kwa wahalifu wanaowashambulia wafuasi wa Jubilee Kaunti ya Mombasa.

Sonko amesema kuwa kuna baadhi ya magenge yanayodaiwa kufadhiliwa na viongozi wa upinzani, ambayo yamekua yakiwasumbua wafuasi wa Jubilee jijini humo.“Kuna baadhi ya wahalifu ambao nina uhakika wanafadhiliwa na viongozi wa upinzani, ambao wamekua wakiwasumbua wafuasi wa Jubilee,” alisema Sonko.Akizungumuza katika uwanja wa Tononoka siku ya Jumapili, Sonko alisema magenge hayo yanafadhiliwa na kiongozi fulani katika Kaunti ya Mombasa, ila hakumtaja.“Kuna kiongozi anafadhili wahalifu hao ili kuhatarisha maisha ya wafuasi wa Jubilee,” alisema Sonko.