Spika wa bunge la kaunti ya Kisii Okerosi Ondieki ameagiza kamati ya sheria katika kaunti hiyo kufuatilia ombi la wanakandarasi wa kaunti hiyo na kufikisha ripoti bungeni ifikapo mei 2, 2016.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni baada ya wanakandarasi wa kaunti hiyo kuandikia bunge la kaunti ya Kisii barua ya kutaka wizara ya pesa katika kaunti hiyo kuchunguzwa na kuchunguza utajiri wa maafisa wa wizara hiyo kwa madai ya utumizi mbaya wa pesa.

Akizungumza siku ya Jumanne katika vikao vya bunge, Ondieki alisoma barua hiyo na kuagiza kamati ya sheria kuchunguza ombi hilo na kulifuatilia kisha kufikisha ripoti kamili kwa bunge hilo.

Kulingana na barua ya wanakandarasi hao, wanalalamikia jinsi kandarasi hutolewa na jinsi pesa hupeanwa kwa wanakandarasi.

“Naagiza kamati ya sheria kufanya uchunguzi wake na kufuatilia ombi la wanakandarasi ili uwazi kuonekana kisha baadaye jibu halisi litapatikana,” alisema Ondieki.