Spika wa Bunge la Seneti Ekwee Ethuro amewataka maseneta na magavana kushirikiana ili kuhakikisha mfumo wa ugatuzi unafaulu nchini, ikizingatiwa kuwa ni mara ya kwanza kutumika.
Ethuro amesema ili kuwa na mafanikio katika ugatuzi, ipo haja ya kuwa na ushirikiano mkubwa baina ya viongozi hao wa kaunti.
Akizungumza katika hoteli moja mjini Mombasa wakati wa ufunguzi wa kongamano la wakuu wa chama cha wahasibu nchini ICPAK, Ethuro alisema ugatuzi umeleta mafanikio makubwa nyanjani.
Aidha, spika huyo amepinga uvumi kuwa maseneta wana uhasama na magavana, kwa kusema kuwa hakuna tofauti yoyote iliyoko baina yao.
Hatahivyo, Ethuro amewataka magavana kuwa na uwazi na ukweli kuhusu matumizi ya fedha katika kaunti zao.
Vilevile, amewataka kufika katika vikao vya kamati ya seneti inayokagua matumizi ya fedha katika kaunti zao wanapohitajika.