Huku zoezi la usajili la wapiga kura linaloendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini linapotarajiwa kukamilika kote nchini, spika wa bunge la kaunti ya Nyamira Joash Nyamoko amejitokeza kuwarahi wakazi wa kaunti yake kuhakikisha kwamba wanajitokeza kwa wingi ili kusajiliwa.
Kwenye mahojiano mapema Jumanne, Nyamoko alisema kuwa yafaa wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuhakikisha kwamba wamesajiliwa na tume ya IEBC kupokea kadi za kupiga kura kwa maana ni haki yao.
"Inashangaza sana kwamba kwa mda huu wote idadi ndogo sana ya watu ndio waliojitokeza kusajiliwa kama wapiga kura na ndio sababu ningependa kuwahimiza wakazi wa kaunti ya Nyamira kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa kama wapiga kura kwa maana ni muhimu sana," alisema Nyamoko.
Nyamoko aidha aliongeza kuwahimiza wakazi wa kaunti hiyo ambao huenda wakafungiwa nje kwenye zoezi hilo kuhakikisha kwamba wanatembelea ofisi za tume ya IEBC ili kusajiliwa.
"Kwa wale labda watafungiwa nje kwenye zoezi hilo litakalo kamilika leo hii wangali na fursa yakusajiliwa kwenye ofisi za IEBC kwani zoezi hilo lingali linaendelea," aliongezea Nyamoko.
Picha. Wananchi wakipiga kura. Spika wa bunge la Nyamira Joash Nyamoko amewahimiza wakazi kuhakikisha wanajisajili kama wapiga kura. Maktaba