Spika wa Bunge la Kaunti ya Mombasa, Thadius Rajwayi pamoja na mwakilishi wa wadi ya Junda Paul Onje, wameachiliwa huru baada ya kukamatwa wakati wa maandamano dhidi ya Tume ya IEBC.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiandamana na Mbunge wa Mvita Abdullswamard Nassir, Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi na Mbunge wa Jomvu Badi Twalib, Gavana wa Mombasa Hassan Joho aliwaongoza wafuasi wa Cord waliokuwa kwenye maandamano hayo kuwatoa wawili hao kwenye kituo cha polisi cha central jiji Mombasa.

Haya yalijiri baada ya maafisa wa polisi kutibua maandamano yaliyokuwa yameandaliwa siku ya Jumatatu na muungano wa Cord kushinikiza kubanduliwa kwa Tume ya IEBC.

Wawili hao walikatwa kwa kuanzisha maandamano hayo kwa mara ya pili, baada ya polisi kuyakatiza mara ya kwanza, hatua iliyopelekea maafisa hao kuwatia mbaroni.

Akizungumza na wanahabari baada ya maandamano hayo, Gavana Joho alisisitiza kuwa maandamano hayo yatafanyika kila siku ya Jumatatu hadi pale maafisa hao watakapokubali kubanduka madarakani.