Spika wa Bunge la kaunti ya Mombasa Thudius Rwajay na Wawakilishi wa wawili wa bunge hilo wametiwa nguvuni na maafisa wa polisi baada ya kushiriki maandamano ya kutaka kuvunjwa kwa tume ya IEBC.
Viongozi hao watiwa nguvuni siku ya Jumatatu mjini Mombasa baada ya kuagizwa kutowachochea wakaazi kuzua rabsa wakati wa maandano hayo na kukaidi agizo hilo kisha kutiwa nguvuni.
Viongozi hao watatu pamoja na wakaazi wanne wanatarajiwa kuandikisha taarifa kwa kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa kicha kufikishwa mahakamani baadaye kujibi mashhtaka hao ya uchohcezi.
Maafisa wa kupambana na ghasia mjini Mombasa wanashika doria kuhakikisha kuwa usalama wa mji huo umeimarishwa ili kila mkenya kuisha kwa amani.