Afisa katika Sekta ya Elimu Kaunti ya Kisii Henry Onderi amesema sharti mkutano katika sekta hiyo ukiongozwa na wanasiasa ufanywe ili kutafuta suluhu ya mikasa ya moto katika shule za Kisii.
Akiongea na Waandishi wa Habari mnamo siku ya Jumatatu katika mji wa Kisii, Onderi alisema ili mikasa ya moto kutafutiwa suluhu katika shule za Kisii sharti sekta ya elimu na wanasiasa kutoka eneo la Kisii kuwa na mkutano ili kutafuta suluhisho ya kudumu ya mikasa ya moto ambayo inaendelea kushuhudiwa katika shule mbali mbali.
Wakati uo huo, Onderi alisema kuwa umoja kati ya wahusika wote wa shule kushirikiana na wanasiasa kama njia mojawapo ya kuzuia mikasa baada ya kuweka mikakati kabambe kati yao.
“Mkasa wa moto ukitokea katika shule zetu suluhu sio kufunga shule na kuwaruhusu wanafunzi kuenda nyumbani, ila jibu halisi lastahili kutafutwa kwa kuwa na kikao maalumu kutafuta jibu la mkasa wa moto huo,’’ alihoji Onderi.
Aidha, Afisa huyo alisema kuwa mikasa inapotokea uchunguzi unastahili kuanzishwa ili kubaini chanzo cha moto huo kutokea na kuwajulisha watu chanzo cha mikasa kama hizo na kutakuwa rahisi suluhu kutafutwa kwa mikasa za aina hizo.
Mikasa ya moto imeathiri baadhi ya shule zilizoko Kisii Shule ya Wavulana ya Cardinal Otunga ikiwa mojawapo na ile ya St. Peters Nyamesocho iliyochomeka jana ambapo Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae alisema uchungunzi uanzishwe kubaini chanzo cha mikasa ya moto hiyo katika shule za Kisii.