Susumila, msanii tajika kutoka Mombasa anayetamba na kibao kipya Wewe, alichomshirikisha kidosho Avril kutoka Nairobi, amesemekana kuamua kuachana na mkewe Kibibi Salim al maarufu 'Chiriku' baada ya miezi kumi na moja ya ndoa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Susumila anasemekana kuachana na mkewe, wiki chache tu baada ya Kibibi kujifungua mtoto wa kike.

Katika mahojiano na blogi ya Ommydallah.co.ke kutoka Pwani, Kibibi alikiri kuachana na Susumila, ila hakutaka kuweka sababu zilizowapelekea kuchukua hatua hiyo.

Duru kutoka kwa jamaa za karibu wa wawili hao, zinasema kuwa wawili hao wamekuwa wakikosana na kutofautiana kwa muda kabla ya kuafikia uamuzi huo.

Susumila alifunga pingu za maisha mwezi Oktoba tarehe 22, mwaka jana katika harusi iliyohudhuriwa na wasanii mbalimbali kutoka Mombasa.