Hatimaye Susumila, msanii tajika kutoka Mombasa amezungumzia kuvunjka kwa ndoa yake na mkewe Kibibi Salim.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye mahojiano na kituo cha Coast Enews, Susumila alikiri kuwa haijakuwa rahisi kwake tangu kutengana na Kibibi.

Alisema kuwa mengi yalisemwa kwenye mitandao na mengi yamezungumziwa kwenya radio na hata televisheni, huku akiongeza kuwa lazima mahasimu wake kwenye ulingo wa sanaa wawe wameshatoa mitazamo yao ambayo amesema huenda ikawa imewapotosha mashabiki wake.

“Katika maisha ya ndoa huwa kuna vitu hutokea na mara nyingi sio mapenzi ya wana ndoa kukosana. Nina uhakika kila mtu akiulizwa kama angependa ndoa ivunjike, hakuna anayeweza kusema kuwa yuataka. Mimi nilionelea kuwa uhusiano wetu hauwezi endelea tena na kama ni sheria za dini yetu nimefanya kinachohitajika. Kwa sasa nitakuwa nje ya uhusiano kwa mda kwani singetaka kufanya uamuzi wa haraka,” alisema Susumila.

Susumila kwa sasa anatarajia kutoa ngoma mpya aliyomshirikisha Timmy Tdat.