Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi nchini NLC Mohammad Swazuri amepinga madai kuwa anashirikiana na mabwenyenye katika kuendeleza unyakuzi wa ardhi nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza jijini Mombasa siku ya Jumamosi, Swazur alisema kuwa jukumu lake kubwa ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata ardhi zao wala sio kuwanyanyasa kwa kuwanyanganya ardhi zao.

“Ningepeenda kuwaomba wananchi kutotilia manani dhana hizo kwani ni porojo tu za kuniharibia jina,” alisema Swazuri.

Kauli hii inajiri baada ya kuzuka madai kuwa mwenyekiti huyo wa Tume ya Ardhi nchini anajihusisha na mabwenyenye katika kuiba ardhi za walalahoi.