Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi nchini NLC Mohammed Swazuri ameipongeza serikali ya Kaunti ya Mombasa kwa kuzindua ruwaza wa 2035.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea katika hafla ya uzinduzi huo siku ya Jumamosi, Swazuri alitoa wito kwa viongozi wengine wanaopinga mradi huo kutoa ushauri zaidi badala ya kutoa pingamizi kwa mradi huo.

Mwenyekiti huyo pia amewasihi wakaazi wa Mombasa kuunga viongozi wa kaunti mkono katika kutekeleza miradi hiyo, huku akisema kuwa miradi nyingi ya serikali hupingwa na wananchi kwa ajili ya ardhi.

Hata hivyo, Swazuri alisema kuwa lazima wote ambao watatoa ardhi zao kwa minajili ya miradi hizo kutekelezwa wapewe fidia ili wawe na makaazi mbadala.