Wanaume kutoka kaunti ya Kisii wameombwa kubadilisha hali yao ya maisha hasa vyakula wanavyokula na vinywaji wanavyovitumia ili kujiepusha kupatwa na magonjwa kama ya saratani ya kibofu.
Akiongea na wanahabari kuhusu ugonjwa huo, daktari Ondari Matoke amesema kuwa wanaume wengi wanaoathirika na ugonjwa huo hunyamaza badala ya kutembelea vituo vya afya na kupata matibabu mapema.
Daktari Ondari amesema kuwa tabia ya kula nyamachoma na kunywa vileo vikali pia huchangia wanaume wengi kupata ugonjwa huo wa saratani ya kibofu.
Tabibu huyo ametaja lishe bora, kuepukana uraibu wa kunywa pombe na kupimwa lila mara vili kubaini ikwa kuna chembechembe za saratani mwilini kama baadhi ya mbinu zitakazowawezesha wanaume kuepukana na hata kukomesha kero la ugonjwa wa saratani ya kibofu, amabao alilelezea luwa tishio kubwa, haswa kwa wnaume wenye umri wa makamo.
Amewahimiza wanaume kufika kwenye vituo vya afya bila aibu yoyote na kujua hali yao ya afya kwa sababu ugonjwa huo ukitambuliwa mapema hutibiwa kwa urahisi.