Kamishina mkuu wa maswala ya usalama eneo la Nyanza Francis Mutie ametahadharisha  wale wanaowalaghai waumiuni kanisani kwa kuwapora pesa. Akizungumza katika chuo cha Leba cha Tom Mboya jijini Kisumu wakati walipozindua rasmi mkutano wa kwanza wa kila mwaka wa maswala ya kidini,Mutie amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa  yeyote atakayepatikana akijihusisha na uhalif huo. Aidha amewataka wazazi kuwapa watoto wao mwelekeo bora kama njia moja ya kuwapa watoto hao mwelekeo wa kidini ili kusitisha visa vya uhalifu. Kwa upande wake mkurugenzi wa Lake basin Centre region for Theology profesa Jack Kameruka ameitaka serikali kuweka mikakati ya kukabiliana na mchipuko wa makanisa yanayoanzishwa kila mara na lengo la kibiashara.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!